Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza, maulamaa 33 mashuhuri wa Pakistan kutoka madhehebu mbalimbali, chini ya umoja wa “Mutahida Ulama Mahadh,” wametoa tamko la pamoja wakitangaza kuwa matumizi ya bidhaa za Israeli ni “haramu kisharia” na wakatoa onyo kuwa: kutumia bidhaa hizo kunahatarisha imani ya Waislamu.
Katika taarifa hiyo ya kihistoria, maulamaa hao walieleza kuwa katika mazingira ya sasa, kutumia bidhaa yoyote inayohusiana na utawala wa Israeli ni kosa kubwa la kidini na ni dhambi. Wamesisitiza kuwa kutoa msaada wa kifedha hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa utawala unaomwaga damu ya Waislamu wasio na hatia, ni sawa na kushiriki katika dhulma na uhalifu.
Taarifa hiyo ilieleza: “Kupiga marufuku bidhaa za Israeli si wajibu kisharia tu, bali pia ni kipimo cha imani na ghera kidini kwa Waislamu duniani. Muislamu yeyote anayeendelea kununua bidhaa hizi, anatakiwa ajue kuwa anaiweka imani yake katika hatari kubwa.”
Maulamaa wa “Mutahida Ulama Mahadh” pia waliitaka serikali ya Pakistan kutangaza rasmi marufuku ya uingizaji wa bidhaa za Israeli au zile zinazotoka katika kampuni zinazounga mkono utawala huo. Walisisitiza kuwa ukimya wa serikali unatafsiriwa kama ushiriki wake katika uhalifu huo.
Maoni yako